TSAH

Masharti ya Matumizi — TSAH

Tanzania Schools Academic Hub · Toleo Juni 2026

Masharti haya yanaongoza matumizi ya mfumo wa Tanzania Schools Academic Hub (TSAH) na shule zilizojisajili. Kwa kukubali masharti haya wakati wa usajili, shule inathibitisha kuelewa na kufuata vigezo vilivyo hapa.

1. Kukubali Huduma

Shule inakubali kutumia TSAH kwa ada na mpango uliokubaliwa na Ofisi Kuu TSAH. Huduma inajumuisha usimamizi wa wanafunzi, walimu, malipo, matokeo, mawasiliano na ripoti.

2. Wajibu wa Shule

  • Kuhakikisha taarifa za wanafunzi, walimu na wazazi ni sahihi na zinasasishwa.
  • Kupata idhini ya wazazi kwa SMS, barua pepe na data ya watoto.
  • Kulinda akaunti za walimu — tumia nenosiri imara na usishiriki na watu wasio na ruhusa.
  • Kulipa ada ya usajili kwa wakati ili huduma zisisimamishwe.
  • Kutumia mfumo kwa madhumuni ya elimu pekee, si kwa shughuli haramu au zisizo za kimaadili.

3. Arifa na Mawasiliano

Barua pepe ya usajili itatumika kwa OTP, idhini ya ombi, kumbusho la malipo, maboresho na arifa muhimu kutoka TSAH. Shule inakubali kupokea arifa hizi kama sehemu ya huduma.

4. Faragha na Data

TSAH inachakata data kwa madhumuni ya elimu na usimamizi wa shule. Soma Sera ya Faragha kwa maelezo zaidi kuhusu uhifadhi na matumizi ya data.

5. Huduma “Kama Ilivyo”

Mfumo unatolewa “kama ulivyo”. TSAH inajitahidi uptime na backup, lakini shule inapaswa kuweka nakala za ripoti muhimu na kufanya uhifadhi wa data za ndani inapohitajika.

6. Kusitishwa au Kufungwa kwa Akaunti

TSAH inaweza kusimamisha au kufunga akaunti ikiwa malipo yamechelewa, taarifa ni za uongo, au kuna ukiukaji wa masharti haya.

7. Mabadiliko ya Masharti

TSAH inaweza kusasisha masharti haya. Mabadiliko makubwa yatatangazwa kupitia mfumo au barua pepe ya shule.

Soma kuhusu mfumo · Faragha · Ingia